Wahamiaji 57 waokolewa na Polisi wa forodha za Italia

Wahamiaji hamsini na saba wameokolewa na polisi wa forodha za Italia na walinzi wa pwani na kupelekwa katika kisiwa cha Lampedusa, kulingana na shirika la habari la ANSA la nchini Italia.

Wahamiaji hao walikuwa ndani ya mashua iliyozuiliwa karibu na kisiwa kidogo cha Lampione kisichokuwa na wakazi.

Walichukuliwa na kupelekwa Lampedusa hapo jana Jumamosi. Shirika la habari la ANSA limesema wahamiaji hao huenda wakawa ni wa kutoka nchini Tunisia.

Waziri wa mambo ya ndani wa Italia Matteo Salvini anaepinga wahamiaji, anajigamba kwa kupungua idadi ya wahamiaji wanaoingia nchini humo, kutokana na juhudi zake za kuwazuia waokoaji kuwasaidia wahamiaji katika bahari ya Mediterania.

Wahamiaji wengi wanaotumia njia ya baharini wanaingia Italia bila ya msaada.