Waziri wa Elimu awapa neno Wanafunzi wanaoenda kusoma China


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako amewaasa wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya Elimu ya juu nchini China kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania nchini humo.

Waziri Ndalichako amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika katika ofisi za ubalozi wa China nchini.

Jumla ya wanafanzi 61 wamepata ufadhili wa masomo kwa shahada za uzamili na uzamivu katika fani za Afya, Uhandisi, Utabibu, TEHAMA na Mazingira.