Wizara ya Afya yasaini Mkataba wa Ushirikiano na Japan


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesaini Mkataba wa ushirikiano katika Sekta ya Afya kati ya Tanzania na nchi ya Japan unaolenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika kuboresha utoaji huduma za afya kwa wananchi.

Mkataba huo umesainiwa mwishoni mwa wiki baina yake na Balozi wa Japan nchini Tanzania Shinichi Goto.

Mkataba huo wa miaka 5 unazingatia maeneo mbalimbali yakiwemo, kuimarisha huduma za Kinga, matibabu ya kibigwa,Uchunguzi ambapo Tanzania itanufaika kwa.kupata vifaa vya kisasa,matumizi ya tiba mtandao katika hospitali za rufaa za mikoa pamoja na kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza