Azam FC yawasili Zimbabwe kuwakabili Triangle United


Timu ya Azam FC kimeshawasili salama mjini Harare nchini Zimbabwe mchana huu, tayari kwa mchezo wa marudiano wa Raundi ya Pili ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Triangle United Jumamosi.

Azam FC watahitaji ushindi wa ugenini wa kuanzia mabao 2-0 Jumamosi Uwanja wa Barbourfields mjini Bulawayo ili wasonge mbele, baada ya kufungwa 1-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam Septemba 15.

Na msafara wa Azam FC uliowasili leo Harare, umefikia katika hoteli ya Cresta Lodge ulitarajiwa kuanza mazoezi leo jioni hadi Alhamisi itakaposafiri kwa barabara kwenda Bulawayo.