Faida za kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako

Biashara nyingi hutumia njia na mbinu mbalimbali kujitangaza ili kuongeza ufahamu wa biashara zao kwa wateja, kuongeza na kupanua solo la bidhaa zao lakini kubwa zaidi kukuza mapato ya biashara husika. Na moja ya njia hizo ni matumizi ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuitangaza biashara yako.

Asilimia 90 ya wataalamu wa masoko wanakiri kuwa mitandao ya kijamii ina nguvu sana katika kutangaza biashara na imekuwa ikionesha matokeo chanya katika biashara zao. Baadhi ya mitandao ya kijamii inayotumika sana katika matangazo ya biashara ni kama Facebook, Instagram, Twitter, Blogs, youtube, linkedin, n.k

Mitandao ya kijamii sasa imekuwa nguzo muhimu sana kama moja ya mikakati inayotumika ya kutangaza biashara na biashara zisizotumia  mitandao ya kijamii inakosa fursa muhimu na makini sana katika kupanua masoko ya biashara zao.


Faida za kutumia  mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako;

Inachangia kufahamika zaidi kwa biashara yako.
Mitandao ya kijamii ni moja ya njia za kutangaza biashara yako kwa gharama nafuu zaidi na inauhakika wa kuwafikia wateja wengi zaidi, kwani asilimia kubwa ya watu wengi sasa hivi wanatumia muda mwingi sana  katika mitandao ya kijamii hivyo kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako kutakuongezea idadi ya wateja na watu wenye ufahamu wa kutosha kuhusu biashara yako kwa ujumla.

Inapanua wigo wa kupata wateja wapya tofauti na wale wanaokuzunguka
Kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutangaza biashara yako  kunakuongezea wigo wa wateja wapya ambao ni vigumu kufahamu kuhusu biashara yako kwani wako mbali na eneo  la biashara husika lakini mitandao ya kijamii inakupatia nafasi ya watu wote watakao kutuna na tangazo la biashara yako kuifahamu na kushawishika kutumia  bidhaa zao na hivyo kugeuka wateja wa biashara yako.

Inajenga uhusiano wa karibu na wateja wako.
Kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara yako na wateja wako hii inasaidia kuweka ukaribu wa kusikiliza maoni, shida na kutafuta ufumbuzi kiurahisi wa kero za wateja wako kwani kwa urahisi kabisa wanaweza kuwasilisha maoni yao kupitia akaunti za biashara yako  za mitandao ya kijamii.

Inaongeza imani na uaminifu wa watu kwenye biashara yako.
Moja ya malengo ya kila biashara ni kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa bidhaa za biashara hiyo, hivyo mitandao ya kijamii kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara na wateja wake na urahisi wa taarifa za biashara yako kumfikia mteja inapelekea kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa biashara yako.

Inasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara yako.
Biashara nyingi hutumia fedha nyingi sana kwa ajili ya kujitangaza na hili huonekana. Pale ambapo njia zinazotumika kutangaza biashara husika zinakuwa ni ghali sana na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa biashara husika hivyo kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii kama njia ya kujitangaza inapunguza gharama hizo za kujitangaza na kupelekea kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara husika na kuipatia biashara nafasi nzuri ya kifedha kuikuza zaidi.

Inaongeza ufahamu wa kutosha dhidi ya soko husika na wateja wako
Kupitia ukaribu unaojengekana wateja wako katika mitandao ya kijamii na kujibkujibu comments za wateja wako katika mitandao ya kijamii hii inapelekea biashara husika kupata taarifa za kutosha za soko husika na kuipa nafasi biashara kuwa na taarifa za kutosha za wateja wake na hii inasaidia biashara kufanya maamuzi na kuweka mikakati inayohitajika kwa wakti husika na solo husika.

Hizo ni baadhi ya faida za kutumia mitandao ya kijamii  kuitangaza biashara yako na Kama bado hujaanza kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako ni vema ukaanza sasa kwani unapitwa na mengi ambayo biashara yako ingenufaika kwa kutumia mitandao ya kijamii.