Haya hapa Makundi ya CECAFA U-20


Timu ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) imepangwa kundi B katika michuano ya Afrika Mashariki ya CECAFA mwaka huu yatakayofanyika Uganda yatakayoanza Septemba 21 mwaka huu.

Tanzania imepangwa na Kenya na Zanzibar, wakati kundi A kuna wenyeji Uganda, Sudan, Djibouti na Eritrea na kundi C kuna Burundi, Sudan Kusini na Somalia.

Kwa mujibu wa ratiba, timu tatu za juu kutoka kundi A na B zitasonga mbele hatua ya robo fainali na kuungana na timu mbili kutoka kundi C.