https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mahakama kuu Mbeya yawahukumu watu wanne kunyongwa | Muungwana BLOG

Mahakama kuu Mbeya yawahukumu watu wanne kunyongwa



Na, Baraka Messa, Songwe.

Mahakama kuu kanda ya Mbeya imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu wanne wilayani Mbozi mkoani Songwe baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia kinyume cha kifungu cha sheria 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho 2002.

Jaji wa Mahakama hiyo Dkt. Adam Mambi akisoma hukumu hiyo (leo) jana jumanne septemba 17 mwaka huu alisema mahakama imejiridhisha pasipo kuacha hofu yeoyote kufuatia ushahidi uliotolewa mahakan hapo kutoka watetezi na mashahidi baada ya kujihoji kuhusu lengo na dhumun la washitakiwa hao.

alisema kati ya watu hao  watatu kwa pamoja walishiriki kumua  Vasko Njowela aliyekuwa akifanya kazi ya kuuza duka sehehemu ya Mpemba Tunduma wilayani Momba na kupora fedha shingi miliion Moja (1000,000) mwezi july 25 mwaka 2014 majira ya saa moja na nusu wakati anarudi akiwa amefika getini kwa mwajili wake.

alisema watuhumiwa walimvamia marehemu wakati anaingia getini akiwa anarudi dukani wakiwa na lengo la kumpora begi ambalo aliweka hela, jambo ambalo lilipelekea marehemu kuanza kugombana na mshitakiwa namba mbili ambaye anafahamika kwa majina ya Mozes Kasitu baada ya kuona mtuhumiwa anazidiwa , mtuhumiwa mwingine Nathani Elias ambaye ni mtuhumiwa namba tatu alitoa bunduki na kumpiga marehemu sehemu ya tumboni huku mtuhumiwa namba moja Nathan Elias akimkata na panga marehemu jambo lililopelekea kupoteza uhai wake.

Jaji Mambi alisema kwa upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi kumi akiwepo Rehema Saidi ambaye alikuwepo eneo la tukio hilo wakati wanafanya mauaji hayo ambapo aliamuriwa alale chini baada ya kupiga risasi juu huku wakiendelea na mauaji hayo na uporaji wa fedha, ambapo baada ya jeshi la polisi kuwakamata shahidi huyo alifanikiwa kuwatambua washitakiwa wawili ambao ni mshitakiwa namba mbili  Mozes Kasitumkazi wa kilimahewa na mshitakiawa namba tatu Elias Mzumbwe (28) mkazi wa Ihanda baada ya watuhumiwa kuwekwa kwenye foleni ya watu 12 aweze kuwatambua.

alisema ushaidi ushahidi wa Maabala pia ulithibitisha kuwa maganda ya risasi ambayo yaliokotwa eneo la tukio kuwa ndio yaliyotumika katika siraha ambayo alikamatwa nayo mshitakiwa namba moja ambaye ni Nathan Elias (32) mkazi wa mwaka Tunduma akiwa Njombe baada ya maelezo yaliyotolewa na washitakiwa wenzake.

pia aliongeza kuwa maelezo ya awali polisi washitakiwa hao walikiri kuhusika kwenye tukio hilo na na katika matukio mbalimbali katika mkoa wa Songwe huku wakitumia siraha aina ya short gan yenye namba 007700112 wakidai kuwa hununua risasi Zambia.

wakati huo huo Mhakama kuu kanda ya Mbeya pia juzi ili mhukumu kunyongwa mpaka kufa Aman Rabi Kalinga (23)  mkazi wa Kijiji cha Mpanda kata ya Nyimbili kwa  kumua Heroni Kalinga (13)na kuchukua viungo vya sehemu za siri kupeleka kwa Mganga aliyefahamika kwa jina moja la Makamu.

Justin Mshokolwa wakili wa kujitegemewa kutoka Mbeya alisema Mahakama imetenda Haki kutokana na matukio ambayo walifanya washitakiwa hivyo huku wakijua kuwa kuua kwa kukusudia hukumu yake ni kuhukumiwa kunyongwa mpaka kifo.

Nayea Shindani Michael wakili wa serikal alisema kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa wengine ambao wamezoea kukatisha maisha ya bindamu wengine kwa makusudi jambo ambalo ni kinyume za haki za binadamu.

"sisi kama Jamhuri tumeridhishwa na hukumu hii na itakuwa fundisho kwa watu wanaofanya matukio haya ambayo yanazidi kuongezeka kila siku" Michael.