Majeruhi wa moto Morogoro waruhusiwa


Majeruhi watatu kati ya kumi na moja aliokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro wameruhusiwa hii leo.

Mkuu wa kitengo cha uhusiano na huduma kwa wateja hospitalini hapo, Aminiel aligaesha amethibitisha.

Mikdadi Issa na Shabani Abdallah Omari ni miongoni mwa majeruhi wa ajali ya moto Morogoro waliohamishiwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo hii leo wameruhusiwa na kutoa shukrani zao kwa watanzania na madaktari kwa kuokoa maisha yao.