Marekani: Gari lilokuwa limebeba watalii lapata ajali


Ubalozi wa China umethibitisha kwamba basi lililokuwa limebeba kikundi cha watalii wa China limepata ajali na kusababisha vifo vya watu wanne.

Takriban watalii wanne walifariki na 12 kupata majeraha mabaya katika ajali hiyo iliyotokea karibu na Hifadhi ya Kitaifa ya Bryce Canyon katika jimbo la Utah la Marekani.

Waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali za eneo kote Utah Kusini na wanaendelea kupokea matibabu.