Msanii Harmonize kufungua Mgahawa wake


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize ametangaza ujio wa mgahawa wake aliopa jina la Konde Boy Mgawaha

Muimbaji huyo ameeleza hilo kifuatia taarifa aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika 'Kidogo na Kingi Mungu Ndie hutoa na yeye Ndie Kamuumba Masikini na Tajiri...!!!! Hata hapa Nilipo ni kw aneema zake Sitokula na Kusaza ikiwa kuna wengine Kula Yao Ni Yashida Nitagawana Nao,".

Huu utakua uwekezaji wa kwanza nje ya muziki ambao Harmonize atakuwa ameufanya toka Tanzania imfahamu na ni wasanii wachache waliofanikisha kufanya uwekezaji nje ya Muziki wao wanaoufanya.