https://monetag.com/?ref_id=TTIb Nampenda lakini Uongozi umemshinda - Rais Magufuli | Muungwana BLOG

Nampenda lakini Uongozi umemshinda - Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza sababu za kutenguea uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Stephen Kebwe.

Amebainisha hayo leo wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua Septemba 20 mwaka huu, hafla iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam.

”Kebwe nampenda lakini Uongozi umemshinda, Kama kuna Mkoa umenisumbua kuongoza ni Morogoro mambo yakikuwa hayaendi, Kuna wawekezaji wa tumbaku wanataka kukimbia na fedha zao, kila unapogusa hovyo, tukatengua Wakurugenzi mfano wa Malinyi tukadhani yataisha lakini wapi” amesema.

“Mkoa wa Morogoro tulitakiwa tuufanyie Demo tutengue kuanzia Mkuu wa Mkoa hadi Mtendaji wa Kijiji wote halafu tunaweka wapya, aliyekuwa RAS wa pale niliagiza astaafu mapema yeye kazi yake ni kuzungumza na walimu anawatoa Vijijini anawaleta Mjini wale anaozungumza nao vizuri”ameeleza Rais Magufuli.

Ameendelea kwa kusema, "Sasa ukizungumza Mkoa wa Morogoro unagundua RC Kebwe alishindwa kazi, ukipewa Mkoa halafu waliopo chini yako wanafanya mambo ya ajabu maana yake hautoshi, DC na DED wanagombana na haujawahi kusema chochote wala kukemea hautoshi”