Philippines: Lori laanguka kwenye mwamba na kuua watu 15


Watu wasiopungua 15 wamekufa baada ya lori kuanguka kutoka kwenye mwamba katika jimbo la Cotabato Kusini mwa Philippines hii leo asubuhi.

Polisi walisema lori hilo, ambalo lilikuwa limebeba watu 20, iliteleza kutoka barabarani na kuanguka kutoka kwenye mwamba karibu saa nne asubuhi kwenye barabara kuu ya Lamsalome, katika kijiji kcha mji wa T'boli.

Watu 14 walikufa papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa, polisi walisema katika ripoti yake ya awali.

Hata hivyo, Rolly Doane Aquino, mkuu wa shughuli katika ofisi ya mkoa wa kukabiliana na janga na kupunguza hatari huko Cotabato Kusini, alisema idadi ya vifo tayari imepanda hadi 15.