Polisi jamii kuwakamata Wanafunzi wanaotoroka Shule



Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Afisa Tarafa wa Elerai Titho Cholobi amewataka polisi jamii wanaoshiriki kuimarisha ulinzi nyakati za usiku kuanza zoezi la kuwakamata wanafunzi ambao ni watoro na kuwafikisha katika shule zao ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki na kutokomeza tatizo la utoro.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa jengo la utawala linalojengwa katika shule ya sekondari Olasiti iliyopo kata ya olasiti wilaya ya Arusha mjini ambapo  licha ya maendeleo mazuri ya kitaaluma shule hiyo inakabiliwa na tatizo la utoro

Ulobi ametoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara yake na kuwataka wenyeviti wa mitaa kwa kushirikiana na watendaji kata kutekeleza agizo hilo ili kupunguza na kuondoa idadi ya wanafunzi wanaoranda randa mitaani wakati wa masomo.

Hata hivyo ameupongeza uongozi wa shule,bodi ya shule kwa kusimamia vyema mradi wa jengo la utawala ulioletwa na serikali kwa nia ya kuboresha miundombinu ya elimu na kuongeza kiwango cha ufaulu.