RPC Muroto anasa mabasi yakisafirishwa petrol na Diesel


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 72 kwa makosa tofauti likiwamo la kusafirisha mafuta ya Petrol na Diesel katika magari ya abiria kinyume na sheria.

Akizungumza na Waandishi wa habari, ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa polisi, Gilles Muroto, amesema, magari matano ya kusafirisha abiria kwenda vijijini yalikamatwa yakiwa na mafuta ya Petrol lita 1277, na Diesel lita 850, yakisafirishwa pamoja na abiria na mizigo mingine katika Hali ya hatari.

"Katika msako uliofanyika tarehe 20/9/2019 katika kituo Cha mabasi yaendayo vijijini eneo la kikuyu katika jiji la Dodoma yamekamatwa mahari ya abiria matano(5) yakisafirishwa mafuta ya Petrol na Diesel na wanaosafirisha katika njia hatarishi kwenye mahari ya abiria" amesema Kamanda Muroto.

Pia amesema wanamshikilia Jonathan Dastani Temu mwenye (41)ambaye ni mkazi wa Area A kwa kosa la kupatikana na Nyara za Serikali  yenye jumla ya zaidi ya shilingi Milioni Mbili (2,875,000) aliyoipata kutokana na uwindaji haramu.

Anasema walimkamata akiwa na nyama ya Nsya wanne na digidigi mmoja, katika stendi mpya ya Mnadani Kizota ndani ya jiji la Dodoma.

Aidha, Kamanda Muroto ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alihifadhi nyama hiyo  katika mfuko wa plastiki na kuweka kwenye boxi na kusafirisha kwenye basi ambalo linafanya safari zake kutoka  kijiji cha Makamanda wilaya ya Manyoni mkoa wa singida kuingia Dodoma.

Hatahivyo, Kamanda Muroto  amesema wamekamatwa watu tisa (9) kwa makosa ya unyang’anyi  wa kutumia nguvu huku zikakamatwa pikipiki 4 ambazo zimekuwa zikitumika katika kupora watu na zilizokamatwa ni MC.660 AXD BOXER NYEUSI,MC 154 BYG BOXER  nyeusi ,MC.569 BMZ HAOJUE nyekundu na Watuhumiwa wanaandaliwa mashitaka na watafikishwa mahakamani.