TAMWA yashauri Waandishi wa habari kutumia mitandao ya kijamii



Na Thabit Madai,Zanzibar

Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto wamewashauri waandishi wa habari Nchini kutumia mitandao ya kijamii katika kufikisha taarifa zinazohusiana na udhalilishaji na ukatili wa wananwake na watoto unaonekana umekithiri visiwani Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa na Maneja wa Sera na Utetezi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania(TAMWA) Haura Shamte, wakati wa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari juu matumizi ya Mitandao ya kijamii katika kufikisha Taarifa kwa jamii.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Chama hicho (TAMWA) Tunguu Mkoa Kusini Unguja.

Haura Shamte alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuendana na wakati na kutumia mitandao ya kijamii katika kufikisha taarifa zinazohusiana na udhalilshaji na  ukatili wa kijinsia.

“kama Dunia inavyokwenda na sisi waandishi wa habari tunatakiwa kuendana na mabadiliko hayo hivyo niwaombe waandisshi wenzangu sasa tuanze kutumia hii mitandao ya kijamii ambapo wananchi wengi na viongozi wapo huko kufikisha taarifa zinazohusu udhalilishaji na ukatili kwa wananwake na watoto” alisema Haura.

Aliongeze kusema kuwa katika taarifa hizo ambazo waandishi wanatakiwa kuzifikisha kwa wananchi kupita mitandao ziwe zenye kutoa elimu na kukemea vitendo hivyo.

“Kuna habari huwa tunaziona katika mitandao ya kijamii lakini huwa zinaongeza udhalilishaji kwa wanawake na watoto hivyo kama waandishi wakati tunapoandikia katika mitandao ya kijamii tuepuke kuchochea kwa huo udhalilshaji zaidi” alieleza Haura Shamte.

Akiwsilisha mada ya matumizi ya mitandao ya kijamiii kwa wananhabari Mohamed Mazrui alisema kuwa waandishi wa habari hawana budi kutumia mitandao ya kijamii kwa kutoataarifa mbali mbali kwa wananchi.

“Tupo katika jamii ambayo inauchafuzi mkubwa wa matumizi ya mitandao ya kijamii hivyo waandishi wa habari hawana budi kutumia hii mitanndao ya kijamii katika kufikisha ujumbe na taarifa mbali mbali za misingi kwa jamii” alisema Mohamed Mazrui.

Aliongeza kwa kushauri waandishi wa habaria yao kusambaza ujumbe kwa uadilifu kama maadili ya habari inavyotakiwa.

“Tumeshuhudia katika mitandao yetu ya kijamii kuna watu husambaza picha, ujumbe na video ambazo hazina maadili nyinyi kama waandishi tumieni mitandao kama maadili yenu ya habari yanavyotaka” alisema Mohamed Mazrui.

Kwa upande wao waandishi wa habari wenyewe walisema kuwa wamekuwa nyuma katika kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kufiksha ujumbe kwa jamiii.

“baadhi yetu tumekuwa tukitumia mitandao ya kijamii kwa mambo binafsi badala ya kufikisha ujembe wa jamii ili kujitangaza kwa kazi ambayo ninaifanya” alisema mwandishi  wa Gazeti la Majira Mwajuma Juma