VIDEO: Mbunge CCM agalagala chini mbele ya Naibu Waziri


Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Arusha Amina Mollel Amemuangukia Naibu waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Mh William Olenasha amsaidie kutatua changamoto ya shule ya Msingi Lengijave na Olback Wilayani Arumeru, Mkoani Arusha kutokana na shule hizo kuwa na vyumba vya madarasa vichache, mabati kuchakaa, sakafu  pamoja na matundu ya vyoo kwa wasichana na wavulana

Hayo yamejiri katika harambee ya uamaliziaji wa jengo la Ibada katika kanisa la Catholic Kigango cha Lengijave Usharika wa Lengijave ambapo amesema licha ya kuchangia huduma za kiroho pia wanatakiwa kujua kuwa wananchi wanahitaji huduma za kijamii ikiwemo elimu ambapo Naibu waziri wa Elimu alisema serikali itajenga vyumba 2 vya madarasa katika shule hizo mbili na matundu 12 ambapo kila shule matundu sita ambapo jumla  itagharimu shilingi milioni 48  na harambee hiyo ya ujenzi wa kanisa wamepata milioni 22 lakini.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE