Wafanyakazi wawili wa TBS wafikishwa Mahakamani


Wafanyakazi wawili wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mkurugenzi wa kiwanda cha Waadilifu ambae ni raia wa China wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kusaidiwa kuingizwa nchini.