Na Rahel Nyabali, Tabora.
Baadhi ya walimu mkoani Tabora wameeleza kupoteza Imani na benki ya walimu nchini MCB wakidai kutoridhishwa na utendaji wa benki hiyo hasa pale wanapohitaji kuhudumiwa na banki hiyo kama wanachama wake.
Yameelezwa hayo Wakati benki ya walimu nchini MCB ikiwa katika utekelezaji wa kampeni yake iliyopewa jina la Amsha amsha iliyofanyika wilayani Tabora mkoani Tabora iliyolenga kuwahamasisha walimu walejee kuitumia benki hiyo.
Wakizungumza wakati wa kampeni hiyo ya Amsha Amsha iliyowakutanisha viongozi wa chama cha Waalimu ngazi za wilaya pamoja na baadhi ya maafisa kutoka benki ya MCB Peter Sizya ni Mwalimu wa shule ya msingi Bombamzinga amesema ni wakati wa benk kuwajibika ili kufikia malengo yake.
Richard Makungwa ni mkurugenzi mtendaji wa benki ya walimu nchini Sanjali na kukiri mapungufu kadhaa katika benki hiyo ya MCB ametoa wito kwa walimu kushilikiana na benki.
Aidha mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameitaka benki ya Walimu nchini MCB kufanya kazi kwa ushindani ili kuwavutia wateja wengi zaidi.