Waziri mwingine ajiuzulu Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza amepata pigo jingine baada ya waziri mwandamizi Amber Rud kujiuzulu kwa kupinga namna ambavyo anashughulikia suala la Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya-Brexit.

Kujiuzulu kwake kumelifanya kuwa juma baya zaidi kwa Johnson ambae anajaribu kuidhibiti nchi yake iliyogawanyika, katika wakati wa mzozo mkubwa wa kisiasa tangu vita vya pili vya dunia.

Rudd alikuwa mwanachama mwenye siasa za wastani wa serikali ya waziri mkuu wa zamani Theresa May ambae aliridhia Johnson kuchukua nafasi ya Mei katika kipindi cha changamoto ya uongozi wa Uingereza mwezi Julai.

Lakini anasema hawezi tena kumridhia kiongozi huyo kutokana na namna anavyoshughulia suala la Brexit na Umoja wa Ulaya au anavyoshughulia siasa za ndani ya nchi.