Anayedaiwa kuiibia Bank milioni 120 anaswa



Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wa tatu kwa makosa tofauti, akiwamo mtumishi wa bank ya EXIM kwa wizi wa fedha kiasi cha shilingi milioni 120, katika kituo chake Cha kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP Gilles Muroto, amesema wanamshikilia bwana Martini Lazaro (33) mkazo wa Makulu, Jijini Dodoma kwa kosa la kumuibia mwajiri wake kiasi cha shilingi milioni 120, na alikamatwa akiwa Singida.

"Mnamo tarehe 29/8/2019, mtuhumiwa Martini Lazaro, 33, mtunza fedha wa EXIM bank, tawi la Dodoma aliiba fedha kiasi cha 120, USD 9513 na URO 50, baada ya wizi huo alitoroka kwenda mafichoni, baada ya msako tulifanikiwa kumkuta akiwa Singida, kwenye nyumba ya wageni Manonga akiwa na kiasi cha shilingi milioni 37,522,000 Kati ya fedha alizoiba" amesema Kamanda Muroto.

Tukio la pili anashikiliwa bwana Ashraf Sani(31) mkazi wa Nyakato Mwanza, kwa kosa la wizi wa vifaa vya magari kama matairi, kwenye mikusanyiko ya watu Kama vile kumbi za starehe na mikutano na kuiba tairi za magari.

Kamanda Muroto amesema " mtuhumiwa huyo aliingia Dodoma na kupanga chumba kwenye nyumba ya kulala wageni, eneo la Bahi Road na amekutwa na gari alivyokuwa akifanya nayo uharifu, gari no.T. 793 CFN Nissan, pia amekutwa na rimu 9, Matairi 5, jeki 2 na spana" amesema.

Katika tukio la tatu wanamshikilia Isack Okwango, 27, mkazi wa Buzuruga Mwanza na Buguruni Dar es saalam, aliyekuwa akitafutwa kwa  mda mrefu, aliyekamatwa kwenye nyumba ya kulala wageni kwa kosa la uvunjaji na akiwa na vifaa vya anavyotumia kuvunja, ambavyo ni jeki moja, bisibisi, simu tatu, camera moja, laptop aina ya toshba, flash disc na kisu kimoja.

Aidha kamanda Muroto amewaonya watu wanaoingia Dodoma kwa lengo la kufanya vitendo vya kihalifu kuwa hawana nafasi kwani watashughurikiwa na vyombo na husika, amewataka wananchi kutoa taarifa pindi wanapohisi kuna muharifu katika maeneo yao.