BREAKING: Necta watangaza matokeo ya Darasa la saba


Baraza la mitihani la Tanzania (NECTA), imetangaza matokeo ya darasa la saba ambapo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu mtihani huo.

Pia watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu. Matokeo ya jumla yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asilikia 3.78.

Baraza la Mtihani la Taifa (Necta) limesema katika Mtihani wa Darasa la saba uliofanyika Septemba 11, 2019 wamebaini walimu Wakuu, Wasimamizi na walinzi walihusika kufanya udanganyifu

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde ameyasema hayo leo wakati akitangaza matokeo ya darasa la saba na kueleza kuwa katika kikao kilichokaa leo tayari wameshazitaarifu mamlaka za ajira na sheria ili ziwachukulie hatua waliohusika na udanganyifu huo. Ambapo

Dk. Msonde amesema mwanafunzi aliyeongoza Kitaifa ni Grace Manga kutoka Shule ya Msingi Graiyaki Mara, akifuatiwa na Francis Gwagi kutoka Shule ya Msingi Paradise ya Geita.

Amesema kuwa aliyeshika nafasi ya tatu ni Loi Kitundu kutoka Shule ya Msingi Mbezi ya Dar es Salaam, na Victor Godfrey kutoka Graiyaki ameshika nafasi ya nne.