Dk. Shein awaapisha washauri wake aliowateua


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein leo amewapisha Washauri wake aliowateua hivi karibuni.


Walioapishwa ni Bw. Abdalla Rashid Abdalla aliyeapishwa kuwa Mshauri wa Rais Mambo ya Siasa.


Aidha, Dk. Shein amemuapisha Bwana Ali Mzee Ali kuwa Mshauri wa Rais katika Masuala ya Historia na Mambo ya Kale.

Hafla ya kuwapishwa viongozi hao ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid.