https://monetag.com/?ref_id=TTIb Iraq yatoa amri ya kutotoka nje Baghdad | Muungwana BLOG

Iraq yatoa amri ya kutotoka nje Baghdad

Vikosi vya usalama nchini Iraq vilitumia gesi za kutoa machozi dhidi ya mamia ya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika eneo la kati mwa Baghdad hii leo, saa chache baada ya amri ya kutotoka nje kutangazwa mjini humo kutokana na siku mbili za ghasia kali ambazo zimeikumba nchi hiyo, huku kukiwa na maandamano dhidi ya serikali.

Katika saa za usika wa manane, milipuko ilisikika ndani ya eneo lililo na ulinzi mkali la Green Zone mjini Baghdad ambako ni eneo la afisi za serikali na balozi za mataifa ya kigeni.

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani umesema uchunguzi unaendelezwa na kuongeza kuwa hakuna mali ya vikosi hivyo vya muungano iliyolengwa.

Kufikia sasa takriban watu tisa wameripotiwa kufariki na mamia wamejeruhiwa tangu ghasia zilipozuka siku ya Jumanne kati ya vikosi vya usalama vya serikali na waandamanaji wanaoipinga serikali .