Jinsi ya kupata wateja wengi katika biashara


Katika maisha ya mwanadamu kuna changamoto mbalimbali anazoweza kupitia. Leo tuangalie mbinu anayo weza kutumia mfanyabiashara ili kumnufaisha na kuendelea kuipenda kazi yake.

Ukitaka biashara yako iwe nzuri na watu waipende ni lazima;

Uwahudumie wateja wako vizuri.

Uwe na uwezo wa kutatua matatizo ya wateja mfano, kuonyesha wateja jinsi ya kutumia bidhaa (uwezo wa kuwaeleza wateja wako vizuri kuhusiana na bidhaa hizo ili waweze kuzielewa).

Elimisha wafanyakazi wako vizuri ili wajue jinsi ya kuielezea bidhaa yako vizuri  na hasa wajue jinsi ya kumjibu mteja mwenye hasira.

Mfanyakazi mwenye tabia nzuri ana maana zaidi kuliko yule anaye tengeneza bidhaa.

Ni muhimu utoe huduma nzuri kuliko ile inayotolewa na washindani wako katika biashara.

Naomba utambue kwamba huduma nzuri inatofautisha biashara yako na ile ya mshindani na mteja anasababu ya kuendelea kununua kwako.Na huduma nzuri pia ina kuwezesha kuuza kwa bei ya juu kuliko wengine na kukuwezesha kupata faida nzuri zaidi bila kupoteza wateja.

Hivo basi kauli nzuri kwa wateja inakusababisha kupata wateja wengi zaidi na kuendelea kuongeza faida zaidi na ndivyo unavyoweza kuuza zaidi.

Kama huduma ni mbaya mteja anaweza kuacha kununua kwako hata kama ameingia dukani kwako anataka bidhaa yako.

Kumhudumia mteja na kumsikiliza maoni  yake kuna thamani sana katika biashara yako.