Jumla ya makosa 1,853 yameripotiwa kwa mwezi Septemba 2019

Jumla ya makosa ya barabarani 1,853 yameripotiwa mwezi wa Septemba 2019 kupungua ambapo Septemba 2018 yalikuwa 2,741 sawa na asilimia 12.6.

Akitoa taarifa  Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu ya Serikali kitengo cha Takwimu za Makosa ya Jinai Madai na Jinsia Asha Mussa Mahfoudh wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali  kuhusu makosa ya barabarani.

Amesema  miongoni mwa makosa hayo ni pamoja na kutofuata miongozo na kanuni za usalama barabarani , kuzidisha idadi ya watu na mizigo, kuendesha chombo cha moto gari, vespa, pikipiki/fifti bila ya leseni , bima na leseni ya njia.

Pia amesema Wilaya ya Magharibi  B ina idadi kubwa ya makosa ya barabarani 345 sawa na asilimia 18.6 kati ya makosa yote yaliyoripotiwa, na upande wa Wilaya ya Kusini ina idadi ndogo ya makosa ya barabarani yaliyoripotiwa ni 35 sawa na asilimia 1.9.

Kwa Upande wa ajali za barabarani  amesema jumla ya ajali 27 zimeripotiwa mwezi wa Septemba , 2019, waathirika 58 ambao kati ya hao 45 walikuwa ni  wanaume sawa na asilimia 77.6 na wanawake 13 sawa na asilimia 22.4 miongoni mwao waliokufa ni 17 sawa na asilimia 29.3 na waliojeruhiwa 41.

Amesema Wilaya ya Mjini imeripotiwa kuwa na ajali nyingi ambazo nane , zikifuatiwa na Wilaya ya Magharibi A, Wete  na Chake Chake zikiwa na ajali nne kwa kila mmoja,Wilaya ya Wete imeripotiwa kuwa na idadi kubwa zaidi  ya walioathirika ambao ni 17, sawa na asilimia29.3.

Wanaoathirika katika ajali za barabarani  ni pamoja na wanaotembea kwa miguu, wapanda baskeli  , pikipiki, , madereva na abiria.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za uhalifu Zanzibar pia ni mkaguzi wa Jeshi la Polisi Khamis Mwinyi Bakari  amesema elimu inahitajika zaidi kwa madereva juu ya kufuata sheria za barabarani.

Amesema ongezeko za ajali  pamoja na vifo zinasababishwa na madereva kuwa wazembe, kuendesha gari mwendo wa kasi na kila mmoja kujiamuliya mwenyewe anavyotaka pasi kufuata sheria zilizowekwa .

Hivyo amewaomba madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika kwani jamii nayo inahitaji amani katika safari zao.