Kamishna wa operesheni na mafunzo ya jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas akiwa na kamati ndogo ya vyombo ulinzi na usalama wakikagua vipenyo rasmi na visivyo rasmi vinavyotumiwa na wahalifu kutoka nchi jirani ya Msumbiji

Kamishna Wa Operesheni Na Mafunzo Ya Jeshi La Polisi Cp Liberatus Sabas Akizungumza Na Madereva Bodaboda waliopo Mpakani mwa Tanzania na Msumbiji eneo la Mtipesa juu ya kukabilina na Wahalifu Watakaoingia au kutoka nchini msumbiji ila amewaasa Madereva hao kuwa na tabia ya kutoa Taarifa Katika Vituo Vya Polisi Vilivyo karibu yao hasa pale wanapoona Mtu na Kumtilia shaka.(PICHA NA JESHI LA POLISI)

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas akiwa na Kamati Ndogo Ya Vyombo  Ulinzi Na Usalama wakiteta jambo baada ya kumaliza kukagua moja ya kipenyo cha Mtipesa ambacho kilichopo mkoani Mtwara mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. (PICHA NA JESHI LA POLISI)

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas, akiwa katika moja ya mitumbwi eneo la  Kihanga Mkoani Mtwara  inayotumiwa na raia kuvusha watanzania wanaoelekea nchini Msumbiji katika shughuli za kujipatia kipato ila wengi wanaotumia usafiri huo ni wakulima (PICHA NA JESHI LA POLISI)