Kikosi cha Usalama barabarani chaanzisha operesheni maalum ya 'nyakua nyakua'



Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani nchini, Fortunatus Muslim amelazimika kufanya operesheni maalum ya kusimamisha baadhi ya madereva wa mabasi maeneo ya Gairo Mkoani Morogoro kutokana na baadhi ya madereva hao kukiuka kanuni za usalama barabarani huku akiwataka kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha kupunguza speed ya  mwendo ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

Akizungumza mara baada ya kuwasimamisha baadhi ya madereva wa mabasi ambao waliositisha safari zao kwa muda, Kamanda Muslim amesema kuwa kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini hali ambayo husababisha baadhi ya barabara kutereza hivyo ipo haja madereva kuacha kuendesha kwa spidi kali na kujaribu kupita magari mingine bila mpangilio maalum.

Aidha Kamanda Muslim pia alizimika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa mabasi katika stendi  ya mabasi ya Msamvu Mkoani hapa na kuwataka madereva kuacha tabia ya kufanya kazi kimazoea kwani kwa sasa Jeshi hilo lipo katika operesheni maalum inayofahamika kama nyakua nyakua ambayo haitomwacha dereva asiyefuata sheria za usalama barabani.