https://monetag.com/?ref_id=TTIb Maambukizi ya VVU nchini yapungua hadi kufikia asilimia 4.7 | Muungwana BLOG

Maambukizi ya VVU nchini yapungua hadi kufikia asilimia 4.7


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mpango wa taifa wa kudhibiti UKIMWI kwa mwaka 2018/19 mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI katika ukumbi mdogo wa bunge jijini Dodoma.

Akiwasilisha taarifa hiyo hapo jana, Dkt. Chaula amesema kwa mujibu wa utafiti wa hali ya maambukizi ya VVU nchini, kiwango cha maambukiz kitaifa kimeshuka kutoka asilimia 7 mwaka 2003/04 hadi kufikia asilimia 4.7 mwaka 2016/17. Huku akitaja maambukizi kwa wanaume ni asilimia 3.4 na wanawake ni asilimia 6.3.

 “Wizara kupitia NACP inatekeleza mpango mkakati wa nne wa VVU na UKIMWI katika sekta ambao unalenga kutekeleza malengo ya dunia ya 90 tatu (90 90 90) yenye mwelekeo wa kupambana na UKIMWI na yanapaswa kufikiwa ifikapo mwaka 2020 “. Amesema Dkt. Chaula.

Dkt. Chaula amesema katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi Juni 2019 Serikali kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi imetekeleza afua mbalimbali kwa lengo la lengo la kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

Afua hizo ni pamoja na Huduma za Ushauri Nasaha na Upimaji, Huduma za tiba namatunzo kwa watu wanaoishi na VVU, Huduma za upimaji wa wingi wa VVU mwilini, Huduma za Tohara ya kitabibu kwa wanaume, Huduma za kondomu, Huduma za VVU na UKIMWI kwa makundi maalum na Huduma za Habari, Elimu na mawasiliano ya kubadili tabia.