Mabaraza ya usuluhishi yatahadharishwa


Na Ahmad Mmow, Nanyumba

Mabaraza ya usuluhishi ya kata yaliyopo katika wilaya ya Nanyumbu, mkoani Mtwara yameaswa ya sipokee na  kuyatolea uamuzi mashauri yaliyo juu ya uwezo wake.

Tahadhari hiyo ilitolewa jana  na mratibu wa shirika la kutambua sheria na haki za jamii(CHPO), Dikson Mwichaha alipozungumza na Muungwana Blog mjini Mangaka.

Mwichaha alisema ingawa mabaraza hayo yanatakiwa kujikita kusuluhisha migogoro, lakini baadhi ya mabaraza yanapokea, kusikiliza na kutolea uamuzi migogoro iliyojuu ya uwezo wake.Hali inayosababisha migogoro mipya.

 Alionya kuwa hali hiyo isipodhibitiwa kwa kuepuka tabia hiyo, haitashangaza kuona na kusikia baadhi wajumbe wa mabaraza hayo wakiendele kufikishwa mahakamani au gerezani kutumikia adhabu.

Alisema baadhi ya mabaraza yanatolea uamuzi mashauri ya ndoa kwa kuzivunja na kugawanya mali za pamoja za wanandoa. Kitendo ambacho nikosa, kwani hayana uwezo huo.

''Mengine wanadiriki kupokea na kusikiliza mashauri yanayohusu mirathi wakati hayana uwezo huo. Badala yake yanachanganya maana kati ya migogoro ya ardhi na mirathi. '' Wasing'ang'anie kufanya majukumu yasiyowahusu ni hatari kwao,'' alisema Mwichaha.

Alisema kabla ya kuanza kusikiliza mashauri yaanze kujiridhisha kutafuta na kujua mambo muhimu ya shauri husika.  Yakibaini kwamba yapo juu ya uwezo wake yasione aibu kupeleka mashauri hayo kwa mamlaka nyingine.

Mbali na mabaraza, Mwichaha alivitaja vikao vya koo ambavyo vinajivesha uwezo wa kugawa mali za wanandoa baada ya kuvunja ndoa na kugawanya mirathi ni chanzo cha migogoro katika jamii. Huku akiweka wazi njia ya kuepuka hali hiyo niwanandoa na ndugu za marehemu kufungua mashauri ya madai na mirathi mahakamani.

Mwichaha aliwaonya pia makatibu wa ma mabaraza hayo waache kuhodhi madaraka na uamuzi. Kwani wenye uwezo wakutoa uamuzi ni wajumbe wa mabaraza, siyo makatibu.

''Wasijiingize kwenye migogoro inaweza kuwasababishia matatizo na kupunguza imani ya jamii kwa mabaraza hayo. Nijambo la kusikitisha kusikia mwenyekiti wa baraza amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.