Loading...

10/15/2019

Nape nampenda sana, angekuwa hajaoa ningempa hata binti yangu - Rais Magufuli


Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amethibitisha kwa mara nyingine kumsamehe Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye huku akisema kuwa anampenda sana na angekuwa hajaoa angempa binti yake.

 Akitoa maagizo hayo leo Jumanne Oktoba 15, 2019 wakati akihutubia wananchi kijiji cha Kiwalala, Lindi vijijini wakati akienda wilaya ya Ruangwa.

"Nawathibitishia Wananchi wa Mtama Nape nimemsamehe ni kijana wangu na ni Kijana mzuri sana shirikianeni nae, Nape nampenda sana ni bahati mbaya ameoa huku angekuwa hajaoa ningempa hata Binti yangu, kwanza ningepata mbegu nzuri ya Mtoto mrefumrefu hivi"

“Najua hili nimelimaliza Halmashauri ya Lindi Vijijini itaitwa Mtama,Nape shughulikia hili najua Wananchi wako wanakupenda na mimi nakupenda, ulifanya dhambi zako nikakusamehe, Nape nimeshamsamehe sio mtuhumiwa hana dhambi yoyote naomba mshirikiane nae ktk kujenga Mtama mpya“
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger