Rais Magufuli atoa neno kwa wateule wake


Rais John Magufuli amewataka viongozi anaowateua wakawatumikie wananchi bila uonevu huku wakimtanguliza Mungu na kuwasisitiza kuwa kuchafuliwa katika uongozi ni jambo la kawaida na kuwasihi kuwa wavumilivu.

Rais John Magufuli leo Oktoba 20, 2019 wakati anawaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, hafla imefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.

"Kazi hizi ni lazima tuwatumikie wananchi, juzi nilikuwa Mtwara tulikuta malalamiko ya wakulima wa korosho ambao wamedhurumiwa malipo yao tangu mwaka 2016/17 na tulijua ni vyama vya ushirika 10 baada ya kumuagiza Brigedia Jenerali wa TAKUKURU wamebaini ni vyama 32 ambavyo vimewadhulumu watu hao takribani bilioni 1.2 na tayari viongozi 99 wameshashikwa

"Wamesharudisha milioni 255 na Brigedia Jenerali amenihakikishia lazima zilizobaki 'waziteme'. Mnaweza kuona AMCOS na vyama vya ushirika vilivyohusika kuumiza wanyonge ambao wanalima kwa shida," amesema Rais Magufuli.

Leo Rais John Magufuli ameshuhudia kiapo cha wateule wake akiwemo Mathias Bazi Kabunduguru anayekuwa Mtendaji mkuu wa Mahakama, Balozi Ally Bujiku Sakila anayekwenda kuwa Balozi pamoja na Gerald Mweli anayekwenda kuwa Naibu Katibu mkuu, Wizara ya Elimu upande wa TAMISEMI.