https://monetag.com/?ref_id=TTIb Rais wa Liberia George Weah afanya mazoezi na timu ya taifa | Muungwana BLOG

Rais wa Liberia George Weah afanya mazoezi na timu ya taifa


Rais wa taifa la Liberia ambaye ni mchezaji wa zamani wa soka George Weah ameamua kufanya mazoezi na timu yake ya taifa ya Liberia jana Jumatatu ya Oktoba 14 kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2021.

Liberia inajiandaa na mchezo wa mzunguko wa awali dhidi ya Chad wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2021, hivyo Weah amefanya mazoezi na timu yake ya taifa kama sehemu ya kuongeza hamasa ya kufanya vizuri.

Liberia itacheza mchezo huo wa kwanza katika uwanja wa Samuel Kanyon Doe Sports Complex unaoingia watu 35000 nchini Liberia Jumatano ya Oktoba 16 ikiwa inahitaji matokeo chanya ili kusonga mbele kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa Chad.

George Weah ambaye toka 2018 amekuwa Rais wa 25 wa Liberia kwa ushindi wa uchaguzi huru, aliwahi kucheza soka katika vilabu mbalimbali Ulaya kama AC Milan, Monaco, PSG na Man City pia ndio mchezaji pekee wa Afrika aliyewahi kushinda Ballon d'Or (1995).