https://monetag.com/?ref_id=TTIb Ripoti: China yaongoza katika uwekezaji barani Afrika | Muungwana BLOG

Ripoti: China yaongoza katika uwekezaji barani Afrika

China ambayo katika miaka 4 iliyopita imewekeza barani Afrika dola bilioni 72,2 imekuwa ndio nchi ambayo inaongoza kwa uwekezaji wa moja kwa moja barani humo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoandaliwa na shirika la kimataifa la ushauri na ukaguzi Ernest & Young (EY), Kati ya mwaka 2014 na 2018 China imeongoza kwa uwekezaji wa moja kwa moja barani Afrika kwa kuwekeza dola bilioni 72.2.

Katika mataifa ya Afrika yanayozungumza lugha ya kifaransa China iliongoza kwa uweekezaji kwa kuwekeza dola bilioni 34,1 ikifuatiwa na Ufaransa, Marakeni ilishika nafasi ya tatu kwa uwekezaji wa dola bilioni 30.8, Nafasi ya nne ilichukuliwa na umoja wa falme za kiarabu na uwezkezaji wa dola bilioni 25.2.

Miongoni mwa mataifa ambayo yameonekana katika kuongoza kwenye uwekezaji wa moja kwa moja ni  Afrika kusini na uwekezaji wa dola bilioni 10,1 na Uhispania na uwekezji wa dola bilioni 5,4.

Sekta ambazo China imewekeza zaidi ni pamoja na mauzo ya reja reja, miundo mbinu, uchumi, mawasiliano, utalii, vyombo vya habari na teknolojia.

Katika taarifa uwekezaji mkubwa zaidi katika bara ulifanyika nchini Misri dola bilioni 44.8, ikifuatiwa na Afrika kusini dola bilioni 41,7 na Morroko dola bilioni 30.

Baada ya nchi hizo zilizofuatia kwa uwekezaji mkubwa zaidi kimpangilio  ni Nigeria, Kenya na Ethiopia.

Kikanda kanda iliyopata uwekezaji mkubwa zaidi ni Afrika ya kaskazini ikufuatiwa na Afrika ya kusini, Afrika mashariki na mwisho ni Afrika ya magharibi.

Ripoti hiyo imesisitiza kwamba miaka ya hivi karibuni uwekezaji zaidi umefanyika katika teknolojia. Mpaka hivi sasa barani Afrika vimeanzishwa vituo vya teknolojia 600. Afrika kusini, Nigeria na Misri ndio nchi ambazo zimepokea mashirika mengi zaidi ya teknolojia.