Serikali kuvifuta Vyama Hewa vya Ushirika 2000



Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bw.Tito Haule amesema kuwa serikali itavifuta vyama hewa vya ushirika zaidia ya 2000 ambavyo havifanyi kazi licha ya kuwa vimesajiliwa na kutambulika lengo ikiwa ni kupunguza utitiri wa vyama ambavyo havina utendaji wowote.

Akizungumza Maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya  ushirika wa akiba na mikopo iliyofanyika kitaifa mkoani Arusha ,ambapo Mrajisi huyo amesema  kuwa viko vyama hewa vya ushirika   vilivyoanzishwa miaka ya nyuma kwa lengo la kunufaika na mabilioni ya JK lakini kwa sasa haviko .

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na mikopo Tanzania Dkt.Gervas Machimu ameiomba serikali iwapunguzie tozo ya asilimia 1% kwa mwezi wanayotozwa na hazina kuu ili ushirika uweze kukua na kuwakomboa wananchi kiuchumi na kuchangia maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Walimu Moshi vijijini,  Godlisten Kombe amesema kuwa vyamavya ushirika vimekua vikihudumia makundi mbali mbali wakiwemo walimu 3000 ambao wamenufaika na fursa za mikopo.