TRA Geita yakamata Pombe kali ikiwa haijalipiwa Ushuru


Mamlaka ya mapato Nchini TRA Mkoa wa Geita imewakamata watu wanne wakiwemo wafanyabiashara Wawili Mjini Geita kwa kukutwa wakiuza na kusambaza Pombe kali ambayo haijalipiwa kodi aina ya Waka Waka Gin pamoja na Vodca.

Meneja wa TRA Mkoani humo HASHIMU NGODA amesema wamekamata shehena jumla ya katoni 328 aina zote ambapo pombe ya Waka Waka Gin katoni 183 na Kasi Vodca katoni 48.

NGODA anasema vinywaji hivyo vina thamani ya 19,680,000 na ushuru wake wa serikali ni 7,194,138.40 Kama ungekuwa umelipwa kwa njia ya kawaida kwa Mujibu wa sheria.

Amewataja waliokamatwa ni pamoja na la WEREMA MASEKE ambaye katika ukaguzi wa Kawaida wa TRA alikutwa akiwa na katoni 97 za pombe hiyo ambayo ilikuwa haijalipiwa ushuru wa serikali, wengine ni TUNGARAZA CHRISPIN ambaye ni dereva wa Gari yenye namba T396 DFC aina ya Toyota Hilux Mali ya Kampuni ya Kasi Plus (T) limeted ambayo ilikuwa imebeba vinywaji hivyo na Afisa mauzo wa kampuni hiyo MAKASA HAONGA pamoja na mmiliki wa kampuni ya Kongoto Company Limited ambaye ni muuzaji wa vinywaji hivyo mjini Geita.