Waandamanaji 100 wakamatwa Marekani


Waandamanaji wapatao 100 walitiwa mbaroni mjini New York, Marekani siku ya Jumatatu baada ya kusababisha msongamano wa magari na uharibifu wa sanamu mashuhuri la Charging Bull linalopatikana katika barabara ya Wall Street.

Vyombo vya habari mjini humo viliripoti ya kwamba mamia ya waandamanaji waliandamana kutoka eneo la Manhattan hadi Wall Street kuanzia saa nne wakiimba nyimbo za kuhimiza mabadiliko katika hali ya anga ulimwenguni.

Msemaji wa polisi mjini New York akiongea na shirika la Xinhua kupitia njia ya simu alisema kua takribani watu 93 walitiwambaroni kwa tuhuma za kuleta hofu miongoni mwa wananchi.

Maandamano hayo ni baadhi ya maandamano kadhaa ambayo yameandaliwa na shirika la Uingereza Extinction Rebellion kwenye miji 60 kote ulimwenguni.