Waziri Biteko aomba maboresho ya miundombinu Jimboni


Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita na Waziri wa Madini, Doto Biteko (CCM) ameomba Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) pamoja na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuongeza kasi ya uboreshaji miundombinu ya barabara jimboni humo ili kuvutia wawekezaji zaidi.

Biteko ametoa ombi hilo kwenye kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa Geita ambacho pamoja na mambo mengine kimejadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara.

Amesema wakati Serikali inaendelea kuboresha mapori yaliyopo wilayani Bukombe kuwa na hadhi ya kuvutia watalii, ubora wa miundombinu ya barabara utavutia zaidi wawekezaji hivyo mamlaka hizo ni vyema zikatekeleza miundombinu iliyokwisha ingiza kwenye mpango.

Naye Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel
ameshauri mamlaka hizo ikiwemo TARURA kuzingatia vipaumbele vya wawakilishi wa wananchi wakiwemo wabunge zinapokuwa zinatekeleza miradi ya barabara.