Na. Adelina Kapaya
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mwandisi Izack Kamwelwe ametoa pongezi kwa makampuni ya kichina, China Railway Seventh Co LTD, Wu Yi Co Ltd of China kwa kasi ya ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Mpanda Mkoa wa Katavi hadi Mkoa wa Tabora baada ya kufanya ziara ya kushitukiza usiku.
Waziri Kamwelwe amesema amefurahishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hio yenye urefu wa kilometa 242 inayojengwa kwa kiwango cha lami na makampuni hayo mara baada ya kumaliza kukagua barabara hiyo
Alisema licha ya Ujenzi wa barabara hio pia kwa upande wa daraja la Mto Koga ambalo linaunganisha Mkoa ya Katavi na Tabora ambalo likijaa maji wakati wa masika husababisha barabara hio kufungwa kufikia mwezi desemba mwaka huu daraja hilo litakua limekamilika na kuanza kutumika
Hata hivyo, Kamwelwe alifanya ukaguzi wa barabara ya kutoka Itigi Mkoani Singida kuelekea Tabora yenye urefu wa kilometa 85 inayojengwa kwa kiwango cha lami na kuridhika na juhudi wanazozifanya kuhakikisha Ujenzi wa barabara unakamilika
Meneja wa Tanroads wa Mkoa wa katavi Mwandisi Martin Mwakabende amesema kutokana na juhudi wanazotumia watahakikisha barabara inakamilika kufikia Desemba mwaka huu na kubaki kazi ya kuweka alama za barabarani ambayo haitachukua mda mrefu kukamilika.
Mwakabende amesema mwezi Desemba mwaka huu mkandalasi wa kampuni ya kichina China Rallway Seventh Co LTD anatalajia kukabidhi barabara ya kutoka Mpanda kuelekea Uvinza Mkoa wa Kigoma yenye urefu wa kilimeta 35 iliyojengwa kwa kiwango cha lami ambayo iligharimu kiasi cha shilingi billion 57,871 kwa serikali hadi kukamilika kwa barabara hio.
Li Wenlon ambaye ni Meneja wa kampuni ya kichina Wu Yi Co Ltd of China inayotengeneza barabara nyenye urefu wa kilometa 108 kutoka Komanga hadi Kasinde Inyonga kampuni hio imeagiza vifaa vya kutosha kutoka nchi ya Afrika ya Kusini ili kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa barabara hio kwa kiwango cha lami.