Waziri Nyongo aliagiza jeshi la Polisi kumsaka mfadhili wa mtandao wa wizi wa mawe ya dhahabu



Na Timothy Itembe Mara.

Naibu Waziri madini, Stanslaus Nyongo ameagiza Jeshi la Polisi kumsaka na kumkamata mtuhumiwa ambaye anafadhili mtandao wa kuiba mawe ya dhahabu ndani ya Mgodi wa North Mara uliopo Nyamongo.

Akiongea na waandishi wa habari willani Tarime mkoani Mara leo Naibu waziri huyo amesema kuwa serikali ya awamu nya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli haitaweza kuwafumilia mafisadi wanaorudisha maendeleo ya Nchi nyuma.

Nyongo amebainisha hayo baada ya kupokea taarifa kuwa kuna moja ya watuhumiwa wa makosa ya kuiba mawe ndani ya mgodi wa Nyamongo ambaye anatuhumiwa kuwa ndiye mfadhili wa mtandao wa wezi wa mawe ya dhahabu ndani ya mgodi wa Nyamongo na kukosesha serikali mapato alikamatwa hivi karibuni hatimaye akatoroka polisi Tarime.

Nyongo alionyesha kukerwa na kitendo hicho ambapo ameliiagiza jeshi la polisi kumsaka mtuhumiwa huyo pale alipo na kumkamata ili kumfikisha kunakohitajika ili kukabiliana na mkono wa sheria.

“Baadhi ya watuhumiwa wanane wa makosa ya wizi wa mawe ya dhahabu ndani ya Mgodi wa ACACIA hivi karibuni walikamatwa kati ya tarehe 15,09  hadi 23 mwaka huu ambapo wote wamefikishwa katika mahakama ya wilaya mkoani hapa ili kujibu mashitaka yanayowakabili lakini cha ajabu nimeambiwa mfadhili wa mtandao huo alitoroka kituoni polisi namimi naagiza jeshi la polisi kumsaka hadi kumkamata”alisema Nyongo.

Nyongo aliongeza kuwa kati ya watuhumiwa waliofikiishwa mahakamani leo wamo wafanyakazi wa mgodi huku wengine wakiwa wenyeji wa Tanzania kutoka maeneo tofauti tofauti ambapo Naibu huyo ameitaka jamii kuacha tabia ya kujihusisha na uhalifu badala yake wajenge tabia ya kufanya shuguli halali zinazowaingizia kipato.