https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wizara ya Afya yakanusha kuzindua dawa za kuongeza nguvu za kiume | Muungwana BLOG

Wizara ya Afya yakanusha kuzindua dawa za kuongeza nguvu za kiume


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekanusha taarifa iliyokuwa ikisambazwa katika mitandao ya kijamii ikieleza kwamba Waziri Ummy Mwalimu amezindua duka maalum linalouza dawa za kukuza nyeti za kiume.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Wizara imeitaka jamii kupuuza taarifa hiyo sambamba na kukanusha kulifahamu duka hilo na kuwataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo.

Taarifa hiyo ya Wizara iliyotolewa leo, Jumapili, Oktoba 20 imewataka Watanzania kufahamu kuwa Serikali ina utaratibu wake pale viongozi wake wanaposhiriki shughuli za kijamii katika sekta husika na kuongeza kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote.

“Kwa kushirikiana na mamlaka za udhibiti dawa, vifaa tiba, vyombo vya dola na usalama nchini, Wizara inaendelea kuwafuatilia wanaotoa taarifa hizi batili na kufanya utapeli kama huu kwetu wananchi na mara watakapobainika watafikishwa katika mkono wa sheria.” Ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kuwaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwataka pia kuchukua tahadhari na matapeli hao wanaowataka wenye uhitaji kupakua kiunganishi cha mawasiliano au kupiga namba ya simu waliyoitoa kwenye taarifa yao hiyo.