Zaidi ya nyumba 15 mkoa Kusini Unguja zimeathirika na mvua zinazoendelea nchini


Na Thabit Madai, Zanzibar

Zaidi nyumba 15 za wananchi katika  kijiji cha kikungwi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja zimeharibiwa vibaya na upepo mkali ulioambatana na mvua  na kuwaacha baadhi ya wananchi kukosa makazi.


 Tukio hlo la upepeo Mkali lilitokea jana majira ya saa sita mchana licha ya kuezua mapaa na kuharibu miundombinu ya umeme ,kukatika na kung’oka kwa miti na baadhi ya mazao mashambani.


Akitembelea eneo hilo pamoja na kuwafariji wananchi waliopata na maafa hayo Mkuu wa Mkoa wa Kusini  Ayuob Mohamed  Mahamoud aliwataka  wananchi hao kuwa na moyo wa subra na uvumilivu wakati serekali ya mkoa huo inaendelea na taratibu za kufanya tathimin ili kujua namna gani ya kuwasaidia.


Alisema kwa hatua ya awali serekali itahakikisha inawapatia msaada wa makaazi na chakula hadi pale makaazi yao ya kudumu yatakaporejea kawaida.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kati, Hamida Khamis Mussa aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuwa na tahadhari na kutokaa chini ya miti katika kipindi hichi cha mvua na upepo mkali ili kuepukana na maafa yanayoweza kujitokeza.

Nao wananchi waliokumbwa na maafa hayo walieleza na kushtushwa na hali hiyo ambayo wanadai hawakuwahi kuiona kwa kipindi kirefu huku wakisema wanamshukuru mungu kwa kutoleta athari ya kifo.

Baadhi  yao wakiomba serikali kuwasaidia kwa hasara walioipata sambamba na hilo wamepongeza hatuwa ya serikali ya Mkoa na wilaya kwa kufika mapema mara baada ya kupata taarifa hiyo.

Sheha wa sheiya ya kikungwi Mohammed Haji Ushahidi alisema uongozi wa shehia hiyo utaharakisha zoezi la tathmini kwa kushirikiana na maafisa wa mkoa na wilaya ili kuziwasilisha serikalini.

Upepo huo uliovuma kwa muda wa dakika kumi na tano katika kijiji cha kikungwi  umeharibu zaidi ya maeneo manne ya shehiya ya hiyo.