Loading...

11/10/2019

Bondia afariki baada ya kufanya mazoezi


Bondia mmoja wa nchini Australia, Dwight Ritchie amefariki mara baada ya kutoka kwenye mazoezi. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 27, na baba wa watoto watatu alikuwa ana mapambano na Michael Zerafa huko Melbourne.

Promota wake Jake Ellis alisema anasikitika kutangaza kifo cha mwanamisumbwi Dwight Ritchie ambaye amefariki akiwa anafanya kitu ambacho anakipenda.

Ritchie alishindwa mara mbili katika mapambano 21, Hivi karibuni alipigana na Tim Tszyu wakiwa wanawania michuano ya uzito wa juu nchini Australia mnamo mwezi Agosti.

Ikumbukwe kifo cha bondia huyo kimetokea mwezi mmoja baada ya kifo cha bondia wa Marekani kutokea. Bondia wa Marekani alikufa baada ya kupata jeraha kwenye ubongo mara baada ya kupigana na bondia Charles Conwell.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger