Loading...

11/21/2019

BREAKING: Msanii Baba Levo arejea uraiani, Zitto atoa neno


Diwani wa Mwanga Kaskazini (ACT-Wazalendo) Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Chipando maarufu Baba Levo baada ya kuhukumiwa kifungo na kutiwa hatiani kwa kosa la kumshambulia askari wa kikosi cha usalama barabarani hatimae arejea Uraiani.

Kupitia mitandao ya Kijamii ya Kiongozi wa Chama hicho na Mbunge wa Kigoma Ujiji, Zitto Kabwe amesema kuwa "Nahukuru Diwani wetu amerudi uraiani."

"Nashukuru sana kuwa Diwani wetu  ACT Wazalendo amerudi uraiani. Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma imeona adhabu ya kuongeza kifungo mpaka mwaka na siku 2 haikuwa halali," amesema Zitto Kabwe.

"Tutaendelea na hatua za kimahakama kufuta rekodi ya jinai ya Diwani wetu. Baba Levo karibu tuendelee na kazi."‬

Awali alihukumiwa kifungo cha miezi 6 katika Mahakama ya Mwanzo mwandiga alipokata Rufaa katika mahakama ya Mkoa akahukumiwa kifungo cha Mwaka 1 na siku 2 jela na leo ameshinda katika Rufaa yake Mahakama Kuu.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger