DC Mvomero atoa agizo kwa Polisi kuhusu kushughulikia waliowapa mimba wanafunzi


Na. Gerald Nkamia, Mvomero

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mwl Muhamed Utaly amelitaka Jeshi la Polisi wilayani humo kuongeza kasi ya kushughulikia kesi za watuhumiwa wawaliowapa mimba wanafunzi wa kike mashuleni ili waweze kufikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukia mkondo wake.

Akizingumza katika kikao cha ushauri cha Wilaya D.C.C kilichofanyika wiki hii kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya, Mkuu huyo wa Wilaya ameonyesha masikitiko yake Kwa jeshi hilo wilayani humo Kwa jinsi linavyochelewesha kushughulikia kesi hizo kiasi Kwamba kunasababisha wahusika kuweza kutoroka na kupoteza ushahidi.

"O.C.D nikuombe sasa ifikie wakati Ofisi yako iache kufanyakazi Kwa mazoea na ilione kuwa jambo hili ni tatizo kubwa na linahitaji kapatiwa ufumbuzi wa haraka kwani inashikitisha kuona kuwa kati ya kesi 26 ni mtuhumiwa moja tu ndio amehulumiwa na nyingine zote ziko kwenye uchunguzi mbaka lini na siku zinazidi kwenda"

Mkuu huyo wa Wilaya amemtaka Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Wilaya kuhakikisha asimamia ufuatiliaji wa kesi hizo kukamilika kabla ya kumalizika kabla ya mwaka huu kwisha ili hatua za kisheria zichukuliwe na wahusika kupelekwa Mahakamani.

Hatua hiyo ya Mkuu wa Wilaya inafuatia hoja ya msingi iliyotolewa katika kikao hicho ya kuandaa mkakati wa kiwilaya wa kutokomeza mimba mashuleni jambo ambalo linasababisha kushuka Kwa ufaulu Wilayani humo.