Ifahamu historia ya mwanamziki Bryan Adams

Binafsi roho yangu inampenda sana mwanamziki Bryan Adams kutokana na uimbaji mahiri wa nyimbo zake, sikio langu mara nyingi huwa halichoki kuusikiliza ule wimbo uitwao everything I do, I do it for you, vipi nawe mwenzangu huwa unapenda wimbo gani zaidi kutoka kwa msanii huyu?

Novemba 5, 1959 alizaliwa mwanamuziki, mwimbaji, prodyuza, mpiga gitaa, mpiga picha, mwanaharakati na mtoaji kwa jamii raia wa Canada Bryans Guy Adams.

Bryan Adams alizaliwa Kingston Ontario nchini Canada kwa wazazi kutoka Uingereza Elizabeth Watson na Caotain Conrad J. Adams waliohamia miaka ile ya 1950 wakitokea Plymouth, England.

Aliibuka na kuwa maarufu nchini Canada na Marekani mnamo mwaka 1983 wakati akitoa albamu yake ya Cuts Like a Knife.

Haikutosha mnamo mwaka 1984 alikuwa maarufu kupitia albamu yake ya Reckless ambayo ilikuwa na nyimbo kama Run to You na Summer of 69 na wimbo wake wa Heaven.

Mnamo mwaka 1991 aliachia albamu ya Waking Up the Neighbours ambayo ilikuwa na wimbo mahiri sana wa (Everything I Do) I Do It for You.

Kutokana na mchango wake katika muziki Bryan Adams ameshiriki na kupata katika tuzo mbalimbali. Ametwaa tuzo 20 za Juno katika ya 56 alizoshiriki.


Ameshiriki mara 15 tuzo za Grammy, pia ametwaa tuzo ya MTV, ASCAP, American Music na tatu za Ivor Novello. Ameshiriki mara tano katika tuzo za Golden Globe na mara tatu katika Tuzo za Academy.

Mwanamuziki huyo ametunukiwa Order of Canada na Order of British Columbia kutokana na mchango wake katika muziki na kujitolea katika jamii hususani masuala ya elimu.

Mnamo mwaka 2011 aliingizwa katika orodha ya wakongwe wa Hollywood Walk of Fame pia Canada Walk of Fame, awali mnamo mwaka 1998 aliingizwa katika Canadanian Broadcast Hall of Fame na miaka minane baadaye aliingizwa katika Canadian Music of Fame.

Mnamo mwaka 2008 Bryans Adams alikuwa nafasi ya 38 katika orodha ya wasanii wa zama zote katika Billboard Hot 100 wakati wa maadhimisho ya miaka 50.

Bryans Adams ni miongoni mwa wasanii wa Canada wanauza sana kazi zao akiwa ameuza zaidi ya kopi milioni 75.

Mnamo mwaka 2017 aliachia albamu ya Ultimate miongoni mwa nyimbo ni Please Stay na Ultimate Love.

Machi 1, 2019 alitoa albamu ya 14 ya Shine A Light.