Jibu la Mbowe baada ya kuambiwa na Spika Ndugai ni mtoro Bungeni


Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amemjibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyedai kuwa ni mtoro bungeni.

Akizungumza leo Mbowe amesema yeye pamoja na wabunge wengine sita wa chama hicho hawapo bungeni kwa kuwa wanahudhuria kesi inayowakabili katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Jana, Novemba 14, 2019 bungeni mjini Dodoma, Ndugai alisema kambi hiyo inakosa nafasi za mara kwa mara kuuliza maswali kwa Waziri Mkuu kwa sababu ya utoro wa Mbowe.

Mbowe na viongozi wengine wanane wa Chadema kwa pamoja wanakabiliwa na  mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.