Loading...

11/13/2019

Laini za simu zisizosajiliwa kutofungwa


Serikali kupitia Wizara wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, imesema laini za simu ambazo hazitajasiriwa hadi kufikia Desemba 31, 2019 hazitazimwa.

Waziri wa Wizara hiyo Kangi Lugola ametoa kauli hiyo leo bungeni Dodoma wakati akijibu mwongozo wa  Mbunge wa Kavuu (CCM) Dk Pudensiana Kikwembe.

Dk. Kikwembe amesema upatikanaji wa vitambulisho hivyo umekuwa mgumu huku akitolea mfano hali ilivyo jimboni kwake.

“Uandikishaji umekuwa shida na kama tunavyojua mwisho ni Disemba. Naomba kauli ya Serikali ili waweze kupata vitambulisho” amehoji.

Karibu katika maeneo mengi ya ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) hufurika misururu ya watu kuanzia alfajiri na mapema wakitaka japo wapate namba tu waweze kwenda kusajili laini zao za simu kabla ya Desemba 31.KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger