Mfahamu Wayne Rooney kiundani zaidi

Rooney alizaliwa Croxtech mjini Liverpool kwa wazazi Jeanette Marie na Thomas Wayne Rooney. Rooney ni wa asili ya Ireland. Rooney alilelewa katika kanisa Katoliki na wadogo zake Graham na John.

Oktoba 24, 1985 alizaliwa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na klabu ya Manchester  United Wayne Rooney.

Kwa sasa nyota huyo anahudumu na klabu ya D.C United ya nchini Marekani. Taarifa zilizopo ni kwamba Rooney atajiunga na Derby County January 2020. Katika uchezaji wake Rooney amecheza zaidi katika nafasi ya ushambuliaji na amekuwa akitumiwa katika nafasi ya kiungo.

Ana rekodi ya ufungaji katika timu ya taifa ya Englnad na klabu ya Manchester United. Wayne Rooney na Michael Carrick ni wachezaji pekee wa England waliowahi kushinda mataji yote ngazi ya klabu ikiwa na maana ya Ligi Kuu ya England, Kombe la FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Ligi, Ligi ya Europa na Fifa Club World Cup.

Rooney alikuwa akimpenda sana mshambuliaji wa zamani wa Brazil Ronaldo de Lima.