https://monetag.com/?ref_id=TTIb Rais Erdogan aishutumu Marekani kukiuka makubaliano ya kusitisha vita | Muungwana BLOG

Rais Erdogan aishutumu Marekani kukiuka makubaliano ya kusitisha vita

Marekani imeshindwa kutimiza masharti ya makubaliano mwezi uliopita kuwaondoa wanamgambo wa Kikurdi wa Syria kutoka katika eneo la mpaka na Uturuki.

Akizungumza mjini Ankara kabla ya kusafiri kwenda Marekani ambako anapanga kukutana na rais Donald Trump kesho Jumatano, Erdogan amekiri kuwapo na hali ya wasi wasi kati ya mataifa hayo wanachama washirika wa NATO.

Miongoni mwa wasi wasi kati ya Ankara na washington ni ununuzi wa Uturuki wa mfumo wa kisasa wa ulinzi wa angani kutoka urusi pamoja na madai ya uturuki ya kurejeshwa kwa imamu wa dini ya kiislamu Fethullah Gulen ambaye Uturuki inamlaumu kwa kuhusika na jaribio la mapinduzi la mwaka 2016 lililofanywa na kundi la wanajeshi.

Uturuki ilisitisha mashambulizi yake dhidi ya Wakurdi wa Syria wa kundi la YPG, baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano, kwanza na marekani, na kisha na Urusi, yote yakiwa na lengo la kuruhusu wapiganaji wa YPG kuondoka kutoka katika eneo la kilometa 30 katika mpaka na Uturuki.