Serikali ya china kuendelea kushirikiana na Tanzania kukabiliana na vitendo vya ujangili


Na. Edina Mbuule

Serikali ya  China imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kukabiliana na vitendo vya ujangili  wa wanyama waliopo katika hatari ya kutoweka Duniani wakiwemo faru na Tembo  katika hifadhi mbalimbali hapa nchini .

Akizungumza wakati wa kukabidhi vitendea kazi mbalimbali na mbegu za nafaka  kwa wananchi wanaoishi kando kando mwa hifadhi ya Taifa ya Mikumi  katika Kijiji cha Mhenda wilayani Kilosa Mkoani Morogoro, Balozi wa china hapa nchini Wang Ke amesema china inatambua umuhimu wa uhifadhi wa wanyama  na misitu hapa nchini.

Haya ni makabidhiano ya vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta mpakato ,viatu vya kazi kwaajili ya askari wa hifadhi ya taifa mikumi pamoja na mbegu mbalimbali za nafaka kilo elfu 4 kwa lengo la kusaidia jamii inayozunguka maeneo hayo ya hifadhi ili kuachana kabisa na shughuli za ujangili badala yake wajikite katika kilimo.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu, Balozi wa china hapa nchini Wang Ke amesema serikali ya china inatambua mchango wa hifadhi hizo katika kuongeza  pato la taifa na kuahidi kuendelea  kuongeza idadi ya watalii ili waweze kutembelea hifadhi hizo zenye kila aina ya vivutio.

Akipokea vifaa hivyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu amesema serikali itaendelea kusimamiasheria za uhifadhi ili kukabiliana na vitendo vya ujangili vinavyoendelea kufanywa na baadhi ya watu huku akiwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali.

Kwaupande wao kamishna wa  uhifadhi TANAPA kanda ya mashariki Asteria Ndaga na Mkurugenzi wa taasisi ya SUKOS  KOVA Kamshna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Seleman Kova wakazungumzia umuhimu wa msaada huo kwa wananchi hao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Mkuu wa Wilaya ya Kilosa , Adam Mgoyi amesema msaada huo utasaidia wananchi wake hususani vijana kujikita katika kilimo na ulinzi wa rasilimali hizo za taifa badala ya kuendelea na vitendo vya ujangili…….insert adam mgoyi mkuu wa wilaya ya kilosa